Saturday, 29 June 2013

Gauni..

Gauni likiwa kwenye mashono..
Hapo limekwisha na kuvaliwa...

Friday, 28 June 2013

Hereni za kanga..

Hizi ni hereni nilizotengeneza kwa kutumia Kanga.

Karibuni katika blogu yangu mpya ya kazi za mikono yangu..

Ninamshukuru Mungu kila siku kwa baraka alizonipa katika mikono yangu. Mungu amenibariki kumudu kazi nyingi za sanaa ya mikono inayotawala ikiwa ni ya USHONAJI.

Blogu hii itakuwa ikiwaletea kazi zangu mbalimbali za ushonaji wa vitu mbalimbali kama vile Mavazi, Mapazia, Mashuka, Mapambo ya aina zote na vitu vingine vingi nitakavyokuwa nikiendelea kuvigundua.

Karibuni Mlango uko wazi...!!!

Vitambaa tayari kufanyiwa kazi ya sanaa..

    Kola ya shati la kiume...

Shati likiwa katika hatua za mwisho... Wanaume mmepata suluhisho ninashona nguo zote, za kiume (mashati, suruali, suti na kadhalika..) 

 Hadi wakati mwingine..

 Da' Mija.